Ratiba ya Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026: Ratiba rasmi ya michezo ya nusu fainali ya CRDB Federation Cup imetangazwa huku timu nne kubwa zikitarajiwa kupambana kuwania nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo muhimu nchini Tanzania.
Katika hatua hiyo ya nusu fainali, Simba SC itavaana na Coastal Union katika mchezo utakaochezwa Juni 20, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Stadium jijini Arusha.
Mchezo mwingine mkubwa utawakutanisha Azam FC dhidi ya Young Africans SC maarufu kama Yanga SC. Mechi hiyo itachezwa Juni 21, 2026 katika Uwanja wa CCM Kirumba Stadium jijini Mwanza.
Ratiba ya Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026
Simba SC vs Coastal Union
Tarehe: Juni 20, 2026
- Uwanja: Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha
Azam FC vs Yanga SC
Tarehe: Juni 21, 2026
- Uwanja: CCM Kirumba Stadium, Mwanza

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kuona michezo yenye ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zilizofika hatua ya nusu fainali. Simba SC itaingia uwanjani ikiwa na lengo la kutinga fainali huku Coastal Union wakisaka kuandika historia mpya.
Kwa upande mwingine, pambano kati ya Azam FC na Yanga SC linatarajiwa kuwa moja ya mechi kali zaidi kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya vilabu hivyo katika mashindano mbalimbali ya ndani.
Pendekezo la Mhariri:
- Makundi ya Kufuzu AFCON 2027 PAMOJA
- Ratiba ya kufuzu AFCON 2027
- Cameroon Defender Che Malone Shines in Algeria After Major Ligue 1 Award