Arsenal Wabeba Ubingwa wa EPL 2026 Baada ya Miaka 22, Manchester City Wakwama Bournemouth. Hatimaye ukame wa miaka 22 umefika mwisho kwa Arsenal FC baada ya kutwaa ubingwa wa Premier League msimu wa 2025/2026 kufuatia sare ya 1-1 iliyopatikana kati ya Manchester City dhidi ya AFC Bournemouth.
Arsenal Wabeba Ubingwa wa EPL 2026 Baada ya Miaka 22
Arsenal wamefanikiwa kutangaza ubingwa huo wakiwa bado na mchezo mmoja mkononi kabla ya pazia la Ligi Kuu England kufungwa rasmi Jumapili ijayo. Washika Mitutu wanaongoza msimamo wa ligi kwa alama 82 baada ya mechi 37, wakifuatiwa na Manchester City wenye pointi 78.
Matokeo ya Bournemouth vs Manchester City
Katika mchezo huo uliochezwa kwa ushindani mkubwa, Bournemouth walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Eli Kroupi dakika ya 39 kabla ya mshambuliaji wa City Erling Haaland kusawazisha dakika ya 90+5.
FT: AFC Bournemouth 1-1 Manchester City
- ⚽ 39′ Eli Kroupi
- ⚽ 90+5′ Erling Haaland
Sare hiyo ilitosha kuipa Arsenal ubingwa rasmi kutokana na tofauti ya pointi ambazo haziwezi kufikiwa tena na Manchester City katika mchezo uliobaki.
Msimamo wa EPL

Top 2
- Arsenal FC — Mechi 37 — Pointi 82
- Manchester City — Mechi 37 — Pointi 78
Arsenal Waandika Historia Mpya
Ubingwa huo ni wa kwanza kwa Arsenal tangu msimu wa 2003/2004 waliposhinda ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja chini ya kocha wa zamani Arsène Wenger.
Mashabiki wa Arsenal duniani kote wameanza sherehe kubwa kufuatia mafanikio hayo yaliyokuja baada ya kusubiri kwa zaidi ya miongo miwili. Mafanikio hayo pia yanaonekana kuwa ushahidi wa maendeleo makubwa ya kikosi hicho chini ya kocha Mikel Arteta ambaye ameiongoza timu kurejea kwenye ubora wake wa zamani.
Pendekezo la Mhariri:
- UEFA Yamfungia Maisha Kocha wa FC Slovacko
- Ratiba ya Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026
- Makundi ya Kufuzu AFCON 2027 PAMOJA