Taifa Stars Yapangwa na Nigeria Kwenye Kundi L AFCON 2027, Tanzania Tayari Yafuzu Kama Mwenyeji. Timu ya Taifa ya Tanzania, Tanzania national football team, imepangwa Kundi L katika droo ya hatua ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations PAMOJA 2027 sambamba na Nigeria national football team, Madagascar national football team na Guinea-Bissau national football team.
Taifa Stars Yapangwa na Nigeria Kwenye Kundi L AFCON 2027
Hata hivyo, Tanzania tayari imejihakikishia nafasi ya kushiriki AFCON 2027 kutokana na kuwa mmoja wa wenyeji wa mashindano hayo pamoja na Kenya na Uganda. Kutokana na hali hiyo, timu moja pekee kutoka kundi la Tanzania ndiyo itakayopata nafasi ya ziada ya kufuzu kushiriki michuano hiyo.
Kenya na Uganda Pia Wapangiwa Makundi
Kwa upande wa Kenya national football team, wamepangwa Kundi D pamoja na South Africa national football team, Guinea national football team na Eritrea national football team.
Nayo Uganda national football team imepangwa Kundi H sambamba na Tunisia national football team, Libya national football team pamoja na Botswana national football team.

Ratiba ya Mechi za Kufuzu AFCON 2027
Ratiba ya michezo ya kuwania kufuzu AFCON 2027 imepangwa kuchezwa katika vipindi vitatu vya kalenda ya FIFA:
- Mzunguko wa 1 na 2: Septemba 21 hadi Oktoba 6, 2026
- Mzunguko wa 3 na 4: Novemba 9 hadi Novemba 17, 2026
- Mzunguko wa 5 na 6: Machi 22 hadi Machi 30, 2027
Mashindano ya AFCON PAMOJA 2027 yanatarajiwa kuandika historia mpya barani Afrika kwa kuandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu ya Afrika Mashariki. Mashabiki wa soka nchini Tanzania sasa wanasubiri kwa hamu kuona namna Taifa Stars itakavyofanya katika kundi hilo lenye ushindani mkubwa licha ya kuwa tayari imefuzu moja kwa moja kama mwenyeji/Taifa Stars Yapangwa na Nigeria Kwenye Kundi L AFCON 2027.
Pendekezo la Mhariri:
- Arsenal Wabeba Ubingwa wa EPL 2026 Baada ya Miaka 22
- UEFA Yamfungia Maisha Kocha wa FC Slovacko
- Ratiba ya Nusu Fainali CRDB Federation Cup 2026