Kikosi cha Senegal cha Kombe la Dunia 2026: Timu ya Taifa ya Senegal ‘The Lions of Teranga’ imetangaza kikosi cha awali cha wachezaji 28 kitakachojiandaa kwa mashindano ya 2026 FIFA World Cup.
Majina makubwa kama Sadio Mane, Kalidou Koulibaly, Ismaila Sarr pamoja na Edouard Mendy yamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha awali kilichotangazwa na kocha Pape Thiaw.
Senegal inatajwa kuwa miongoni mwa timu zenye uzoefu mkubwa kutoka Afrika kuelekea Kombe la Dunia 2026 huku kikosi hicho kikichanganya wachezaji wenye uzoefu na vipaji vipya vinavyoendelea kung’ara barani Ulaya.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kikosi hicho kitapunguzwa kutoka wachezaji 28 hadi 26 kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano hayo makubwa duniani.
Senegal ipo Kundi I katika michuano ya Kombe la Dunia 2026 pamoja na France, Norway na Iraq.
Kikosi cha Senegal cha Kombe la Dunia 2026

Goalkeepers: Mory Diaw (Le Havre), Yehvann Diouf (Nice), Edouard Mendy (Al-Ahli).
Defenders: Ilay Camara (Anderlecht), Krepin Diatta (Monaco), El Hadji Malick Diouf (West Ham United), Ismail Jakobs (Galatasaray), Kalidou Koulibaly (Al-Hilal), Moustapha Mbow (Paris FC), Antoine Mendy (Nice), Moussa Niakhaté (Lyon), Mamadou Sarr (Chelsea), Abdoulaye Seck (Maccabi Haifa).
Midfielders: Lamine Camara (Monaco), Pathé Ciss (Rayo Vallecano), Habib Diarra (Sunderland), Idrissa Gana Gueye (Everton), Pape Gueye (Villarreal), Bara Ndiaye (Bayern Munich), Pape Matar Sarr (Tottenham).
Forwards: Assane Diao (Como), Bamba Dieng (Lorient), Nicolas Jackson (Bayern Munich), Sadio Mané (Al-Nassr), Ibrahim Mbaye (Paris Saint-Germain), Cherif Ndiaye (Samsunspor), Iliman Ndiaye (Everton), Ismaila Sarr (Crystal Palace).
Pendekezo la Mhariri:
- Makundi ya FIFA U-17 Kombe la Dunia
- Tanzania Yapangwa Kundi Gumu Kombe la Dunia U-17
- Taifa Stars Kwenda Morocco Kwa Mechi za Kirafiki